MABADILIKO YA KANUNI ZA MKOPO WA 10%…

Katika kuhakikisha ufanisi zaidi wa mikopo ya 10% kwa vikundi vya wanawake, vijana na Watu wenye walemavu itolewayo ya Halmashauri, Serikali imelegeza masharti ya kukopa mikopo  hiyo kupitia mabadiliko ya kanuni, 2021.

Kanuni mpya ambazo zimeanza kutumika kuanzia mwishoni wa Mwezi Februari zinaelekeza mabadiliko katika:

  • Nambari ya wanakikundi katika vikundi vya wanawake na vijana kutoka 10 mpaka 5 huku watu wenye ulemavu kuwezeshwa hata mtu mmoja kutoka watu wa 5.
  • Kila halmashauri zimeelekezwa kutenga kiasi cha fedha ili kuwawezesha maafisa maendeleo jamii kufanya tathmini na ufatiliaji wa mikopo iliyotolewa.

Kwetu UNA Tanzania na wadau wengine ,haya ni mapinduzi makubwa, kutokana na kazi kubwa tunayoifanya katika eneo hili. Tunaamini kanuni hizi zitasaidia kuwezesha vikundi vingi zaidi kunufaika na mikopo hii na kuleta tija na uendelevu kwa jamii.